Go to content
 

Swahili/Kiswahili

Jinsi huduma ya kisheria yaweza kukusaidia

Twaweza kukusaidia kutatua  shida mbali mbali za kisheria kama kesi za  jinai, kuvunjika kwa jamii, msaada wa malezi, kuathiriwa kiakili, vita vya  kinyumbani, madeni, makaazi, ulinzi wa raia na huduma ya uhamiaji.

Zifwatazo ndizo huduma zetu  za kisheria za bure: 

  • Maelezo kupitia kwa simu 
  • Mawaidha ya uso kwa uso kupitia daraka 
  • Machapisho, semina na warsha tofauti tofauti

Ukihitaji mawaidha mengine kuliko hayo ya kisheria, unaweza kuuliza kiri ya huduma ya kisheria. Kupata kiri italingana na hali yako. 

Kupata usaidizi piga simu kwa LawAccess NSW katika nambari ya simu ifwatayo – moja tatu sufuri sufuri nane nane nane tano mbili tisa kujua vile tunaweza kukusaidia. 

Ukihitaji mtu anayezungumza lugha yako, piga simu kwa idara ya utafsiri nambari moja tatu moja nne tano  sufuri (kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni). Uliza mtafsiri akuunganishe na LawAccess NSW kwa nambari ya simu moja tatu sufuri sufuri nane nane nane tano mbili tisa.